Manchester United imemuongeza mlinzi wa Brighton Ben White kwenye orodha ya wachezaji wa beki wa kati wanaowataka. Anajumuishwa na wachezaji wengine wa Kifaransa Dayot Upamecano,22, wa RB Leipzig, na Raphael Verane wa Real Madrid 27. (MEN)
Hatahivyo, matumaini ya United kumsajili Upamecano mwezi Januari pengine yanaweza kuwa yamekwisha baada ya kuondolewa kwenye ligi ya Mabingwa. (Express)
Paris St-Germain wanajiandaa kwa uhamisho wa mkopo mwezi Januari wa kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli na inaamini Spurd wamejiandaa kumuachia mchezaji huyo wa miaka 24. (Mail)
Matumaini ya United kumsajili Upamecano mwezi Januari pengine yanaweza kuwa yamekwisha baada ya kuondolewa kwenye ligi ya Mabingwa
Chelsea itahitaji kumfanya David Alaba mchezaji wao anayelipwa kitita kikubwa kama watatakiwa kumrejesha Stamford Bridge beki huyo wa pembeni wa Bayern Munich.(Mirror)
Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana mpango wa kumsajili mlinzi wa Uhispania Eric Garcia,19 kutoka klabu ya zamani ya Manchester City. (Sun)
Mshahara wa kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen huko Inter Milan huenda ukamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kupunguzwa bei ya kurudi Ligi Kuu. (Telegraph - subscription required)
Kushindwa kusonga mbele kwa Red Bull Salzburg katika ligi ya mabingwa kumeongeza matumaini ya Arsenal kumsajili kiungo wa kati Dominik Szoboszlai mwezi Januari.(Football.London)
Hatahivyo, washika bunduki wanatarajia kukabiliana na upinzani kutoka kwa RB Leipzig, huku Bayern Munich na Real Madrid wakifikiriwa kuvutiwa naye. (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg Dominik Szoboszlai
Arteta ana matumaini ya kuendelea kumbakisha Folarin Balogun katika klabu ya Arsenal. Mkataba wa mshambuliaji huyo utamalizika msimu ujao. (Metro)
West Brom wameanza kubainisha mbadala wa kocha Slaven Bilic, ambaye huenda akapoteza ajira yake ikiwa kikosi chake kitapigwa na Newcastle siku ya Jumamosi. (Mail)
Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema mabingwa hao wa ujerumani hawahitaji kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Halaand,20, kwasababu wana mashambuliaji wa Poland Robert Lewandowski,32. (Tuttosport - in Italian)
Mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 23, amesema anataka kusalia Manchester United wakati wote wa ajira yake.(Times)
Aston Villa itahitaji kuimarisha uchaguzi wao wa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji mwezi Januari kama mshambuliaji Wesley, 24, hatarejea kutokana na jeraha (Mail)
Manchester United wanatathimini mafanikio ya uamuzi wa uhamisho kwa mkopo, wakati vijana kadhaa wa klabu hiyo wamekuwa na wasiwasi wa kukosa muda wa kucheza. (MEN)
Wachezaji wakubwa wa United wanahofia hali isiyowiana ya timu hiyo kwa kutokana na mabadiliko kadhaa ya kiufundi na uchaguzi yanayofanywa na kocha Ole Gunnar Solskjaer. (Telegraph - subscription required)
Mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 23, amesema anataka kusalia Manchester United wakati wote wa ajira yake.(Times)
Mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi na Arsenal Robin Van Persie amesema alimisihi kocha wa wakati huo Arsene Wenger kumsajili beki wa kati Muitaliano anayekipiga Juventus Giorgio Chiellini,36, kuisaidia Arsenal kushinda taji la ligi ya Primia. (Effe Relativing, via Metro)