Klabu ya ligi kuu Marekani inaongoza kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa kiungo wa kati Mjerumani anayekipiga Arsenal Mesut Ozil,32. (DHA-in Turkish)

Juventus na AC Milan pia watakuwa wakimuwania mchezaji huyo mwenye miaka 27. (Calciomercato - in Italian)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga ameiambia klabu ya Rennes kuwa anataka kuondoka msimu ujao. Mchezaji huyo mwenye miaka 18 anavutiwa na Manchester United.(Mundo Deportivo via Sun)

Juventus wanaweza kumuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey msimu ujao baada ya mchezaji huyo mwenye miaka 29, kushindwa kuisaidia klabu yake tangu ajiunge nayo akitokea Arsenal mwaka 2019. (Mail)

Mshambuliaji wa Brazil Hulk, 34, anaweza kujiunga na klabu ya ligi ya primia kwa uhamisho huru mwezi Januari baada ya kumaliza mkataba wa miaka minne na Shanghai SIPG ya China. (Sun)

Kurejea kwa Samuel Umtiti katika kikosi cha Barcelona baada ya kujeruhiwa ni hatua moja nyingine kuelekea kuiacha klabu hiyo mwezi January, wakati Everton na Juventus zote zikivutiwa na mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi, 27. (Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa Everton ya Italia Moise Kean, 20, amefungua milango kwa uhamisho wa kudumu kuelekea Paris St-Germain baada ya kuanza vyema na mabingwa hao wa ufaransa . (Goal)

Leeds United wameendelea kumfuatilia Marcus Edwards,22, baada ya winga huyo wa kushoto kuondoka Tottenham na kujiunga na Vitoria Guimaraes ya Ureno mwaka 2019.(Football Insider)

Klabu kadhaa za ligi ya Primia zinavutiwa na kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Vesga,27, ambaye mkataba wake na Athletic Bilbao utakamilika msimu ujao.(AS - in Spanish)

Bristol City ni miongoni mwa vilabukadhaa vinavyopanga uhamisho kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto George Cox, 22, aliyekuwa kwa uhamisho wa kudumu akitokea Brighton kwenda Fortuna Sittard ya Uholanzi msimu uliopita.(Football Insider)