Muigizaji wa filamu Tanzania, mzee Jengua amefariki dunia leo Jumanne Desemba 15, 2020 Mkuranga mkoani Pwani.

Taarifa iliyotolewa na katibu wa chama cha waigizaji Mkoa wa Dar es Salaam, Doricy Kente inaeleza kuwa mke wa msanii huyo amethibitisha kifo hicho.
 
Mzee Jengua alipata umaarufu mkubwa katika mchezo wa runinga wa Kidedea uliokuwa ukirushwa na kituo cha ITV na kutayarishwa na Chemchem Arts Group, akiigiza kama mzee katili na mwenye roho mbaya.
 
Mbali ya kuwa kuigiza marehemu Mzee Jengua alikuwa na kipaji cha kuchezea nyoka, alikuwa akifanya maonesho sehemu mbalimbali, pia ni mfugaji wa kuku.

Mungu aiweke roho yake mahali pema.