TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 leo Desemba 22 imepoteza mchezo wa hatua ya fainali ya Cecafa  iliyoanza kufanyika Desemba 12 nchini Rwanda na kuwa washindi wa pili.

Tanzania ilitinga hatua ya fainali baada ya kupata ushindi kwa penalti 4-3 dhidi ya Ethiopia, mchezo uliochezwa Desemba 20 nchini Rwanda mbele .

Kwenye fainali ya leo dakika 90 zilikamilika kwa Uganda kushinda mabao 3-1 Uwanja wa Rubavu,Rwanda.


Licha ya kupoteza mchezo wa leo Timu ya Taifa ya U 17 imekata tiketi ya kushiriki Afcon 2021 nchini Morroco.