Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema zoezi la kuwaapisha wabunge 19 wa viti maalum wa Chadema lilifuata utaratibu kwa upande wake na kwamba kinachoendelea na sinema tu.

Spika Ndugai ameyasema hayo leo Desemba 8, jijini Dodoma, kwenye hafla ya uapishwaji wa wabunge wawili walioteuliwa na Rais Dk. John Magufuli hivi karibuni.

Wabunge hao ni Dk. Dorothy Gwajima ambaye pia ani Waziri Mteule wa Waizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mhandisi Leonard Chamililo.

“Tuendelee tu kuwa wavumilivu, tuangalie hiyo sinema ambayohaijawahi kutokea katika nchi yoyote ile duninia.

“Kwamba Spika unaambiwa wafukuze wabunge 19 wanawake alafu unauliza kos lao nini? unaambiwa kosa lao sababu waliitikia wito wako wa kuja kuwaapisha kwako alafu na wewe ukawaapisha, hivi duniani kote mliwahi kuona wapi kitu kama hicho?

“Kwa sababu kwa njia ya wale na wengine wa viti maalum ina njia mbili kwanza ni njia ya Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC) kuniandikia na kusema kuwa hawa wansstahili kuwa wabunge, waapishe na huondiyo utaratibu na ulifuatwa nikawaapisha.


“Njia ya pili huwa ni majina yanayopita kwa kutangazwa kwenye gazeti la serikali, gazeti la serikali lilikwisha wapitisha kwa kuwatangaza kwa kuwa orodhesha kwa majina mmoja mmoja katika hao 19.

“Kwa kuwa hayo yametekelezwa ipasavyo na Spika naye kawaapisha, alafu mtu mwingine anasema kosa la hao ni wewe kuwaita na kuwaapisha kwa hiyo wafukuze, hivi na mimi si nitaingia kwenye Guiness Book (Kitabu cha rekodi za dunia) kama Spika wa ajabu kabisa ambaye hajawahi kutokea duniani, kuwafukuza wabunge kwa kosa la kuwaapisha,” amesema Spika Ndugai.

Ameongeza kuwa: “Kwa hiyo tamthilia siku hizi Watanzania wanapenda tamthilia kwa hiyo nayo ni tamthilia tuendelee tu kuiangalia inavyokwenda, lakini kwa aajili tu ya wananchi ufuatiliaji wa jambo hili kama kuna walakini mahalisiyo kwa spika nalo lina ruti mbili au zaidi.

“Moja kufuatilia tume ya uchaguzi, sababu wao ndio wanaratibu masuala yote ya uchaguzi na kuniletea mimi, mimi siyo kazi yangu akichaguliwa mbunge niende nikaulize watu kwamba huyu ndiye mbunge aliyechguliwa hakuna, mimi nakaa hapahapa Dodoma mimi nitaletewa na Tume, kwa hiyo majina yote tuliyoletewa na tume tayari tumeyafanyia kazi na kwa upande huo hakuna shida.

“Sehemu ya pili kama jamaa zetu wanasahau ni mahakamani, ambayo ndiyo inaweza kuniambia kuwa kuna walakini kwa mbunge flani kwa hiyo chukua hatua hii, hakuna njia nyingine kwa kosa hilo labda kama kosa jingine, kosa kwamba kwa nini waliapishwa sasa wewe ulitakaje?

“Bahati mbaya au nzuri wameapishwa, hayo mengine tamthilia tuwaachie wenyewe ziendelee kama kawaida, njia hizo mbili ndizo ambazo kama hawafahamu utaratibu zinaweza kuwa saidia kuweza kutatua matatizo yao ya ndani ambayo mimi siyo shughuli yangu kuendelea nayo, vinginevyo niseme kwamba wabunge wote ambao mmeapishwa wote endeleeni na kazi zenu za kibunge popote mlipo na sisi tunaendelea na ukarabati ndaninyabukumbi wa bunge kuna baadhi ya maeneo, vitendea kazi tumekwisha wapa,” amesema Spika Ndugai.

Spika Ndugai ameongeza kuwa: “Tutakapofika hapa Februari 2, 2021 tutaanza na kwa wiki moja na mjadala wa hotuba ya Rais Dk. John Magufuli aliyoitoa hivi karibuni, hotuba ile ni nzuri…nzuri sana ni dira, kwa hiyo Watanzania wengi watapenda kusikiliza uchambuzi na kuelekea kutekeleza uono wa serikali katika miaka mitao inayokuja.

“Lakini pia wiki ya pili tutakuwa na mjadala wa mipango kuelekea bajeti ya 2021/22,” amesema Spika Ndugai.

Kauli hiyo ya Spika inakuja baada ya kuwapo kwa sintofahamu baada ya Chama ch Demokrasia na Maendeleo Chadema kutangaza kuwafta uanachama, Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kinyume na utaratibuwa Chama hicho.