Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Hamis Taletale  ambaye pia ni meneja wa Msanii Diamond Platnumz afunguka juu ya kutowahi kuzuia Media kupiga nyimbo za wasanii wa WCB.

Akizungumza leo kupitia XXL ya Clouds Fm, Tale ameeleza kuwa hawajawahi kuzia media yoyote kutokupiga ngoma za wasanii wao bali Media ya Clouds ndio walianza.

“Hatujawahi kuzuia media yoyote kucheza nyimbo za wasanii wetu, uhalisia ni kwamba nyie (Clouds) ndio mlianza, na ninajua mmewahi kutusapoti na mlishawahi kuamua kutokutoa sapoti,” alisema Tale.

Majibu hayo yalimuibua Mtangazaji wa XXL, Adam Mchomvu, ambapo alisema, “Hatujawahi kuacha kukusapoti,”

Babutale akaendelea, "Tukienda kwenye uhalisia mimi na wewe (Adam) tumeshawahi kukutana kabla hata Marehemu hajafa, ukaniambia #Tale kwanini msikae na viongozi mkamaliza, nikakuuliza kwamba kwani tumekosa nini tuseme tumalize.

"Shida tulikuwa tunataka kujua kwa nini hawapigi tumekosa nini.” alimalizia @babutale .