Imefahamika kuwa msanii Shilole yupo kwenye penzi zito na mpiga picha aitwaye Rommy, ambaye ni mpenzi wake wa zamani lakini waliachana miaka 11 iliyopita.

Rommy mwenyewe amethibitisha hilo ikiwa leo Disemba 20, 2020 ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Shilole, ambapo ameeleza kuwa waliwahi kuwa na mahusiano huko nyuma kisha wakaachana.


''Nichukue nafasi hii ya siku yako ya kuzaliwa Shilole kukwambia kua Nakupenda Sana Darling na nashukuru Mungu kwa kutukutanisha tena kwenye maisha yetu ikiwa kila mmoja wetu ameshatimiza malengo yake'', ni sehemu ya ujumbe wa Rommy kwa Shilole.


Rommy amesema penzi lao limerejea, baada ya ndoa zao wote kuvunjika hivi karibuni na walipokutana wakaongea na kurejesha mapenzi yao.