Sony Music Ent. Afrika imemteua Christine Mosha maarufu Seven kuongoza upande wa Masoko na Maendeleo ya Wasanii kwa Ukanda wa Afrika Mashariki

Mosha ambaye ni Mtanzania atakuwa na jukumu la kuijenga Kampuni hiyo ikiwemo kukuza Wasanii wa Afrika Mashariki na kuwafanya wafanye vizuri ndani na Nje katika level za Kimataifa na atakuwa anaripoti moja kwa moja kwa Sean Watson, Managing Director wa Sony Music Afrika .


“Seven ametumia karibu maisha yake yote kutoa mchango kwenye Muziki wa Afrika , ana passion , na anafaa kuutangaza Muziki wa Afrika Mashariki kwenye Ramani ya Dunia”- Sean Watson


Hivi karibuni Msanii Ommy Dimpoz alitangaza rasmi kuwa ameingia Mkataba na Sony Music Ent. Afrika.