MSHAURI wa Yanga kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu hiyo, Senzo Masingiza, amefunguka juu ya kuondoka kwake hapa nchini na kurejea kwao Afrika Kusini.

Imekuwa sio kawaida kwa Senzo kutokuonekana viwanjani wakati Yanga ikiwa inacheza ambapo hivi karibuni hakuonekana katika michezo miwili ambayo Yanga walicheza ndani ya wiki moja dhidi ya Dodoma Jiji na Ihefu.

Akizungumza na Spoti Xtra, moja kwa moja kutoka nchini Afrika Kusini, Senzo alisema kuwa ameondoka Tanzania na kurudi Afrika Kusini kwa ajili ya kujumuika na familia yake ikiwa pamoja na kuzungumza mambo mbalimbali ya kifamilia kipindi hiki cha sikukuu.“


 
Nimekosekana katika michezo miwili tu ya Yanga ambayo timu ilicheza ndani ya wiki moja, kwa sasa nipo nyumbani Afrika Kusini ambapo nimekuja kuiona familia yangu na kuijulia hali.“

Nashukuru kuona kuwa mambo yanaendelea vizuri, jambo zuri ni kuona kuwa kuna furaha kwenye familia, mimi naendelea vizuri, nipo salama, hivyo nitarejea hivi karibuni nchini Tanzania,” alisema Senzo.