Kwa wapenzi wa kapo ya mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, hii ni zaidi ya habari njema kwao, IJUMAA linakupa ubuyu ulionyooka.

Taarifa mpya zinaeleza kuwa, ni rasmi chaguo la sasa la mama mzazi wa Diamond au Mondi, Sanura Kassim ‘Sandra’ katika ishu ya ndoa ya mwanaye huyo ni bibie huyo wa Kiganda anayeishi Durban nchini Afrika Kusini.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo makini kutoka ndani ya familia ya Bi Sandra au Mama Dangote, kimepenyeza ubuyu ‘exclusive’ kwa kusema kuwa, mama huyo humwambii kitu kwa sasa kwa Zari na tayari ‘ameyapika’ kwa mwanaye ili aweze kurudiana na zilipendwa wake huyo waliyezaa naye watoto wawili; Tiffah Dangote na Prince Nillan.

FULL KUWASILIANA

Chanzo hicho kimeeleza kuwa, siku za hivi karibuni, Mama Mondi amekuwa akiwasiliana kwa karibu mno na Zari na wapo kwenye hatua nzuri kuweza kufufua penzi lililokufa kwa takriban miaka miwili na ushee.

“Zari hana neno kabisa na kama mlifuatilia, alipotinga Bongo hivi karibuni kuleta watoto, alikuwa tayari kwa lolote, lakini tatizo lilikuwa ni Mondi ndiye alikaza,” kilisema chanzo hicho.

MIPANGO NI MWAKANI

Kikizidi kuweka mambo sawa, chanzo hicho kilisema kuwa, kwa sababu mazungumzo ya Zari na Mama Mondi yapo kwenye hatua nzuri, suala la ndoa linaweza kuwa mapema tu, mwakani (2021).

“Unajua Mondi naye ndiye alichelewesha huu mchakato kwa sababu Zari hakuwa na hiyana, ninahisi kwa sababu Mondi alikuwa na ishu ya yule mwanamke wa Uarabuni ndiyo maana alikuwa anasitasita, lakini kwa sasa naona hata yeye amelainika. “Kama unavyojua Mondi huwa hapindui kwa mama yake, anamsikiliza sana hivyo kwa hili nalo ni kama meza boga zimazima.”

Baada ya kusindikiza na ujumbe huo, Zari aliingia kwenye eneo la kutoa maoni chini ya picha hiyo kisha akaandika; “Final say.” Kauli hiyo ya Zari iliyomaanisha ‘mtu wa mwisho wa kutoa uamuzi’ ilileta maana zaidi baada ya Mama Mondi kuijibu; “Soon nitatoa tamko, sitaki mchezo.”

‘KODI’ YAFUNGULIWA

Gazeti la IJUMAA lilizungumza na mtu mwingine wa karibu ndani ya familia ya Mama Dangote ambaye alifungua ‘kodi’ hiyo kwa kusema kuwa, mama anamaanisha kuwa atatangaza ‘soon’ kuhusu mwanaye Mondi kufunga ndoa na Zari ambaye wametoka mbali.

kumsukuma mlevi tu, kilichobaki ni kusherehekea tu mwakani maana hata Mondi naye amechoshwa na maisha ya upweke,” kilisema chanzo hicho.

IJUMAA LACHIMBA

Kwenye kuchimba kwake, Gazeti la IJUMAA lilifanikiwa kubaini kuwa Mama Mondi na Zari kwa sasa wanawasiliana mara kwa mara na urafiki wao umerudi kama ule wa zamani wa mtu na mkwewe.

Miongoni mwa ‘doti’ zilizounganishwa na Gazeti la IJUMAA, ni picha aliyoiposti hivi karibuni Mama Mondi akiwa jijini Mwanza alipokuwa na mumewe, Uncle Shamte. Kwenye picha hiyo, Mama Mondi alisindikiza na ujumbe uliosomeka hivi; “Ukituchukia “Usinitaje bwana, lakini habari ndiyo hiyo, Zari anatakiwa sana na Mama Dangote,” kilihitimisha chanzo hicho.

MONDI NAYE…

Kwenye posti zake, Mondi naye amekuwa akionesha kwamba sasa gari limewaka kati yake na Zari kwani juzikati aliaweka picha ya Zari na bintiye Tiffah Dangote kisha akasindikiza na ujumbe uliosomeka; “Roho za mimi.”

MAMA MONDI ANASEMAJE?

Gazeti la IJUMAA lilimvutia waya Mama Mondi ambapo alipokea, lakini hata hivyo, simu yake ilionekana yupo kwenye eneo lenye kele hivyo kushindwa kupata vizuri maswali aliyokuwa anaulizwa. Hata hivyo, jitihada zaidi zinaendelea ili kuweza kumsikia anazungumziaje ishu hiyo.

TUJIKUMBUSHE Zari na Mondi walioishi kwa miaka kadhaa na kujaaliwa watoto wawili, walifikia hatua ya kumwagana baada ya kushindwana tabia.

Zari alimtuhumu Mondi kuwa anafanya matukio mbalimbali na wanawake wengine ambayo yanamdhalilisha yeye pamoja na watoto.

Kabla ya uhusiano wake na Zari, Mondi aliwahi kuwa na uhusiano na warembo wengine wengi akiwemo Wema Sepetu, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Hamisa Mobeto na mtoto wa Kikenya, Tanasha Donna. Kati ya hao, wawili tu ndiyo alibahatika kuzaa nao mtoto mmojammoja ambao ni Mobeto na Tanasha.

Stori: Mwandishi wetu