December 3, 2020 Kapteni Salah Salim Jeizan ambaye ni rubani wa Shirika la Ndege la Kenya Airways amefariki dunia kutokana na Virusi vya Corona.

Imeelezwa kuwa, Kapteni Jeizan (57) aliwasili Uwanja wa Ndege wa Heathrow, London akitokea Kenya na alipata changamoto za upumuaji akiwa hotelini na kukimbizwa Hospitali.

Anakuwa rubani wa pili wa KQ kufariki kwa COVID19 baada ya Kapteni Daudi Kibati kufariki dunia kwa ugonjwa huo mwezi Aprili.

Tangu kuanza kwa mlipuko huo nchini Kenya watumishi mbalimbali wa sekta ya anga wamegundulika na maambukizi.