Msanii wa muziki wa injili Rose Muhando amesimulia mazito aliyowahi kupitia tokaaanze kuimba muziki wa injili ikiwa ni pamoja na kutishiwa bastola na vipigo visivyoisha  na kutaka kukutana na IGP Sirro kusimulia yaliyomkuta.

 "Nimepitia matatizo mengi makubwa kwenye maisha yangu na siwezi kuyazungumza pengine kwa jeshi la polisi labda niwe hana na ana na Sirro ndo nitaongea kila kitu tena na ushahidi kabisa vinginevyo siwezi kuongea mazito niliyopitia kwa sababu ya usalama wangu" Rose Muhando

"Watu wamenitengenezea skendo ili kunichafua kwenye jamii  wamenitangazia ninatumia mada ya kulevya baada ya kukataa utumwa toka kwao na kukubali hata waniue kuliko kuishi kwenye utumwa nimetawaliwa na watu nimepigwa hadi kutishiwa bastola kichwani, sikuwahi kuongea haya kabisa ila leo ninaongea na ujasiri kwakua najua serikali ya sasa hivi si ya mchezo mchezo na walioninyanyasa na kunitishia kuniua awawezi kunifanyia hivyo kwenye utawala huu" Rose Muhando

"Kuna mengi ya kuongea ila siwezi kusema kwenye vyombo vya habari laba nikiwa ana kwa ana na Sirro na naongea hivi sababu najua kuna watu wengi wanapitia utumwa kama wangu na awajapata ujasiri wa kuzungumza

"Kabla ya kuitwa Rose Muhando nilikuwa naitwa Shadya kutoka Kilosa, kwetu mimi ni mtoto wa mwisho, toka nilivyozaliwa ilikuwa kila mwenzi naongezewa damu na hali iliyopelekea kuwa dhaifu sana na nilipofika miaka 9 hali ilikuwa mbaya na nilizunguka kote kwa waganga na sikupona ila tulikuwa na jirani yetu alikuwa ni mtu ambaye ameokoka na akawa ananiomba na napata nafauu, kuna siku niliwaambia wazazi wangu waniache nife na nikataka kulala chumba cha peke yangu na saa tisa usiku niliona mwanga ambao ulikuwa na rangi saba na niliona mkono mweupe umenigusa na ukasema 'Mimi ni Yesu nimekuponya na amka ukanitumikie' na nilipona saa hiyo hiyo na nikarudi shule na ile sauti ikawa inanirudia mara kwa mara, hivyo ilibidi nibadili dini na nikaokoka japo familia yangu haikutaka sababu nimetoka kwenye familia ya kiislam na Baba yangu alikuwa shekhe Mkuu Kilosa hivyo haikuwa rahisi " @malkiarosemuhando #LeoTena