Rapa G Nako Warawara toka Weusi, anasherehekea mwaka mmoja wa ndoa yake na mkewe @jsyasinta.

Ndoa ya wawili hao ambayo imezidi kushamiri tabasamu la furaha kila uchwao, ilifungwa Desemba 28, Kanisani maeneo ya Osterbay jijini Dar es Salaam.

Akisherehekea kutimiza kwa mwaka mmoja wa ndoa na miaka 9 ya wao toka wawe pamoja #GNako kupitia ukurasa wake wa #Instagram, amemuandikia ujumbe huu mkewe @jsyasinta, "Miaka tisa ya kuwa pamoja, mwaka mmoja wa ndoa thank you love, my friend, cha umbea mwenza I love you".

Sanjali na hilo, wanandoa hao wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwae #Gianna.