Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni Amiri jeshi Mkuu amefanya mabadiliko katika Jeshi la Uganda (UPDF) na kumrejesha mwanae, Lt. Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais yaani Special Force Command(SFC)

Mabadiliko hayo yamefanyika wakati wanasisa wa upinzani wakilaumu Jeshi la Polisi kwa kuwasumbua katika kampeni zao za uchaguzi zinazoendelea nchini.

Aliyekuwa Naibu wa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Meja Jenerali Sabiiti Muzeyi na nafasi hiyo imechukuliwa na Gen. Paul Lokech aliyekuwa katika uangalizi maalum wa masuala ya Sudani kusini, ikiwa Sabiiti Muzeyi amerudishwa makao makuu ya jeshi kusubiri kupewa nafasi nyingine.

Naibu wa Msemaji wa Jeshi la UPD Luteni Kanali Deo Akiiki amedhibitisha uteuzi huo.

Jenerali Mhoozi amerudishwa kwenye cheo ambacho aliwahi kukitumikia kabla ya kubadilishwa kuwa mshauri wa rais Museveni katika masuala ya ulinzi.Na kitengo hicho ndicho kina husika na kumulinda rais wa Uganda.

Mabadiliko haya yamefanyika wakati zikiendelea kampeni za uchaguzi mkuu wa rais ambapo wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakituhumu jeshi la polisi kuwatatiza kwenye kampeni zao, lakini Msemaji wa jeshi amesema ni mabadiliko ya kawaida tu.

 

Credit:BBC