Rais Dkt. John Magufuli ameongoza mamia ya waombolezaji kuuaga mwili wa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela aliyefariki dunia Disemba 6 mwaka huu jijini Dodoma.

Shughuli ya kuaga mwili wa Jaji Mstaafu Nsekela imefanyika katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Viongozi mbalimbali wameshiriki katika shughuli hiyo akiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.

Mara baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Jaji Mstaafu Nsekela mwili huo umesafirishwa kwa ndege kwenda mkoani Mbeya kwa mazishi, yatakayofanyika Alhamisi Disemba Kumi.