Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani E. Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Prof. Manya pia ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Prof. Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania.

Uteuzi wa Prof. Manya unaanza leo tarehe 11 Desemba, 2020 na ataapishwa leo mchana Ikulu, Chamwino Mkoani Dodoma.