Kwenye kuadhimisha siku hii ya Ukimwi duniani, kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio imepiga stori na msanii Ferooz ambaye alitoa wimbo wake wa starehe ambao unazungumzia ugonjwa huo.

 

Wimbo huo ulifanya vizuri kwenye kuelimisha kuhusiana na ugonjwa huo mpaka kuzawadiwa gari na Rais wa awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa, akizungumzia kuhusu wimbo huo Ferooz amesema 


"Wimbo wangu ya starehe idea niliitoa kwa Rais wa awamu ya tatu marehemu Benjamin William Mkapa, alitusihi wasanii kutunga nyimbo za kuelimisha watu kuhusu Ukimwi".


"Kila nilipokuwa natafuta mtu ambaye nataka asimame kama Daktari  akili inaishia kwa Prof Jay, kama ningemkosa basi Mwana Fa alitakiwa asimame, hata Prof Jay naye hakujua kama nilikuwa nimejipanga hivyo".


Aidha ameongeza kusema "Napenda apatikane msanii mwingine ambaye atafanya nyimbo ambayo itaishi kama wimbo wa starehe ambavyo umedumu, najua kuna vijana wanaweza kutengeneza vitu vikali vitakavyo kuwa na elimu kwa jamii, ni kitu ambacho sio cha kukurupuka ni kujipanga".