Wananchi wa Kijiji cha Kona Nne Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora wameshangazwa na kurejea kwa mwili wa marehemu aliyefariki kwao na kusafirishwa kwenda Kahama na wakati wakijiandaa kwa mazishi mwili ukarudi kwa mazingira ya tatanishi Kijijini hapo.


Tumezungumza ma Mwenyekiti wa Kitongoji cha King’wangoko Said Nzogola amesema ni kweli mwili huo umerudi na kabla ya kuusafirisha kwenda Kahama ndugu wa marehemu walidai mahari ya binti yao “Waliondoka wameubeba na kaka yake kutoka tumbo moja alikuwepo na walipofika kule nao wakashangaa na baadae jione wakarudi kuchukua mwili tena na mwanzo kabla halijatokea tukio hilo walikuwa wanadai mahari shilingi Mil.1.5” Said Nzogola.