Mwanamuziki Ommy Dimpoz amesaini rasmi kufanya kazi na label ya Sony Music Entertainment Africa yenye makazi yake nchini Afrika Kusini.


Dimpoz amesaini dili hilo leo Disemba 10, 2020. Mkurugenzi wa label hiyo, Sean Watson amezungumza baada ya Dimpoz kumwaga wino, amesema


"Ni wakati wa furaha sana kuwa na msanii wa aina ya Ommy Dimpoz kufanya maamuzi ya kushirikiana nasi Sony. Tunafuraha kuhusu kuunganisha nguvu na yeye ili kuleta muziki mzuri kwenye masikio ya mashabiki wengi tuwezavyo." alisema MD huyo wa Sony Music Entertainment Africa.


Sambamba na dili hilo, Ommy Dimpoz ataachia album yake mapema mwaka ujao, huku mida ya saa 10 Jioni ya leo ataachia wimbo wa kwanza toka kwenye album hiyo uitwao "DEDE"


Akizungumza pia baada ya kusaini na Label kubwa duniani Dimpoz amesema


"Nina furaha na najisikia kuheshimiwa kwa kujiunga na Sony Music Africa, nyumbani kwa wasanii wenye vipaji duniani. Huu ushirikiano ni hatua muhimu sana kwenye safari ya muziki wangu, katika muda sahihi kwenye maisha yangu kuona ukuaji na mabadiliko kwenye muziki wangu."