Mwanamke huyo wa Nigeria ambaye ni daktari wa binadamu ameibuka hadharani kusalimu amri kufuatia ndani ya ndoa yake kupitia manyanyaso mengi na ukatili unaotishia uhai wake toka kwa mumewe huyo. Wawili hao wamezaa pamoja watoto 4 na kwenye ndoa wameishi pamoja kwa miaka 6

Daktari huyo ambaye jina lake ni Ifeyinwa amesema kwa miaka mingi mumewe huyo amekuwa akiendekeza vitendo vya umalaya kubadilisha wanawake kila leo na kesho, hiyo tisa, kumi amesema kwa miaka mingi amekuwa akinyanyaswa kwa vipigo na kuamua kuvumilia ndoa isivunjike labda mwanaume atabadilika

kilichomzindua sasa aanze kunusuru maisha yake ni kwamba ana wiki 4 tu tangu ajifungue mtoto wao wa nne kwa operasheni lakini licha ya mshono alionao anasema mume hakujali alianza kumpiga sana na sababu ya kumpiga ni kuwa mke huyo alimwambia mumewe kuwa kwasasa tayari wana watoto 4 hivyo awe na matumizi mazuri ya pesa badala ya pesa anazopata kuishia kwenda kuzitumia kwa michepuko yake anayobadilisha kila wakati ndio mume huyo akashusha kichapo cha kufa mtu . Mwanadada amesema mimba ilipokuwa na miezi mitatu alipigwa na mume huku akimkalia tumboni

Mume huyo kwa jina la Pius anafanya kazi kwenye kituo cha Channels TV na tayari mwajiri wake ameagiza uchunguzi ufanyike baada ya video ya mkewe kuhusu domestic violence kusambaa