KIUNGO mshambuliaji Mtanzania, Simon Msuva juzi amefanikiwa kupata ushindi wa pili akiwa na timu yake mpya ya Wydad Casablanca katika michezo ya Ligi Kuu ya Morocco (Botola).

 

Msuva alifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya timu yake ya zamani ya Difaa El Jadida huku akiwa sehemu ya kikosi hicho ila alianzia benchi.

 

Wydad wamepata ushindi huo wakitoka kuifunga Youssoufia Berrechid mabao 2-0 anayoichezea beki wa kulia Mtanzania, Nickson Kibabage mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Mohammed.Akizungumzia ushindi huo wa mfululizo, Msuva alisema kuwa: “Huu ni mwanzo mzuri kwangu nikiwa na timu yangu niliyoanza kuitumikia katika msimu huu mpya wa ligi nikitokea Difaa.

 

“Katika michezo hiyo miwili yote nilianzia benchi ni baada ya kuchelewa kujiunga na timu, kwani tangu nimejiunga na Wydad nimefikisha wiki mbili sasa hivi tofauti na wenzangu walianza ‘pre seasson’ pamoja kwa muda mrefu.“Hivyo, Watanzania watarajie kuniona nikiwa katika kikosi cha kwanza katika michezo ijayo.”