Samirah Yusuph
Bariadi.
Naibu mrajis wa vyama vya ushirika udhibiti na usimamizi Collins Nyakunga amekutana na wananchama wa vyama vya ushirika katika mkoa wa Simiyu (SIMCU) na kuwaelimisha juu ya manunuzi ya mfumo wa stakabadhi ghalani.

Amekutana na wanachama hao desemba 16,2020 katika mji wa Bariadi ambapo alisema kuwa malalamiko ya wakulima katika malipo ya mazao, na udanganyifu wa watendaji ni sababu ya kubwa iliyopelekea kubadiri mfumo wa ununuzi kutoka katika pesa taslimu hadi mfumo wa kielectroniki ambapo mkulima atapokea pesa kwa njia ya mtandao. (account ya bank na namba za simu).

Nyakunga alisema kuwa mfumo huo utasaidia kudhibiti udanganyifu pamoja na kudhurumiwa kwa wakulima ukienda sambamba na uuzaji wa mazao kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani.

"Mifumo hii yote ni kuhakikisha kuwa mkulima anakuwa na kilimo chenye tija na anapata faida kwa sababu mazao yanakuwa na udhibiti na udhibiti na hata itakapofika wakati wa malipo mkulima atapata pesa yake bila kupitia kwa mtu yeyote," alisema Nyakunga.

Aidha aliongeza kuwa ili Udhibiti uweze kufanikiwa  ni lazima kushirikiana kwa pamoja kati ya wanunuzi na wakulima  kutengeneza mifumo ambayo itasaidia wananchama wote ili kuhakikisha vyama vinakuwa na manufaa.

Mfumo wa manunuzi wa stakabadhi ghalani ni mfumo ambao ulianzishwa katika msimu wa kilimo wa 2019/2020 lakini haukufanikiwa kutokana na wakulima wengi kushindwa kuuelewa hali iliyosababishwa na kuchelewa kwa elimu ya mfumo huo.

Akifafanua mfumo huo Erick Temu Afisa kutoka bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala alisema kuwa  Mfumo wa stakabadhi ghalani ni mfumo wa mkulima kupeleka mazao kwenye ghala lenye reseni ili kurahisisha uuzaji wa mazao kwa pamoja katika ghala kuu ambalo litauza mazao hayo kwa njia ya mnada.

Hivyo vyama vya ushirika vinatakiwa kuwa Utunzaji wa kumbukumbu kutofautisha na kuchambua thamani ya mazao ya mkulima pamoja na Ubora wa mazao vikiambatana na usahihi wa vifungashio kutokana na mzao  pamoja chapa katika vifungashiona kuvifanyia ukaguzi  wa awali kabla ya kupeleka katika ghala kuu.

"Baada ya mkulima kupeleka mazao katika ghala ataandikiwa Nyaraka ya serikali ambayo inaandika taarifa za ubora wa mazao na mazao yanauzwa kwa njia ya mnada kisha malipo yanafanyika ndani ya saa 48 baada ya mazao kuuza,"Alisema Erick na kuongeza kuwa:

"Faida za mfumo huo ni pamoja na Upatikanaji wa taarifa sahihi katika sekta ya kilimo na inarahisisha katika kukuza soko na mapato ya mkulima vilevile  uhakika wa usalama wa mazao na matumizi ya vipimo rasim hivyo mkulima haibiwi".

Kwa upande wao baadhi ya wakulima mkoani Simiyu walieleza kuwa kilichopelekea mfumo huo kutokutumika katika msimu uliopita ni kile walichokiamini kuwa wanaibiwa kwa sababu hawakuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na mfumo huo.

"Kwa sasa tutawaita wadau wote wa kilimo ili tuhakikishe kila mmoja anapata elimu ya mfumo huu na katika msimu huu ninauhakika tutautumia vizuri,"alisema Emmanuel Mboi makamu mwenyekiti wa SIMCU.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Simiyu Mariam Mmbaga aliwata wakulima kuacha kutumika kwa maslahi binafsi ili kunufaisha baadhi ya vikundi vya watu kwa kivuli cha siasa na kuwa na utayari wa kuyaishi na kuyasimamia maadhimio ili kuboresha mfumo ambao utakuwa na manufaa kwa wakulima na kuwapatia faida.

"taasisi za fedha zihakikishe zinatembelea wakulima na kuhakikisha wanakuwa akaunti za benki ili wote waweze kuwa katika mfumo pamoja na kuwapatia elimu sitahiki lakini katika hili,

Muone umuhimu wa kuwaweka wazi wakulima katika mfumo huu ili kuweza kuelimisha faida na hasara zitakazo patikana kutokana na mfumo".alisema Miriam na kuongeza kuwa:

"Changamoto za ushirika zipo mikononi kwa maafisa ushirika hivyo wanapaswa kutumia nafasi hiyo kuwatendea wakulima na kutenda haki licha ya uwepo wa changamoto kadhaa lakini haiwezi kuwa sababu ya kushindwa kutoa huduma kwa wakulima".

Mwisho.