Jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma linamshikilia mzee wa wa miaka 72, ambaye ni mchungaji wa kanisa la Pentecostal Gospal Mission, lililopo wilaya ya Mbinga kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Simon Marwa Maigwa, amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia mzee huyo aliyefahamika kwa jina la Boston Chimalilo, ambaye alikamatwa Desemba 1, 2020, maeneo ya makaburini akiwa katika harakati za kumuingilia mtoto huyo.

"Wasamaria wema waliokuwa wakipita maeneo hayo ya makaburini walimuona mchungaji huyo akiwa anamepiga magoti akimlazimisha mtoto huyo kufanya kitendo hicho na baada ya mhanga kuhojiwa alikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchungaji huyo tangu 2019", amesema Kamanda Maigwa.