Klabu ya Yanga imemuongezea mkataba kiungo wake Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, kuendelea kukipiga Jangwani, lakini uongozi wa timu hiyo haujaweka ni mkataba wa muda gani.


Niyonzima aliyerejea Yanga katika kipindi cha dirisha dogo msimu uliopita, ameongezewa mkataba huo baada ya awali kuwepo kwa tetesi za kuachwa na kikosi kutokana na kukosa na namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.


“Klabu yetu ya Yanga leo tumeongeza Mkataba na Kiungo wetu Niyozima, Fabregas bado yupo yupo sana jangwani,”. Yanga