Aliyekuwa mshambuliaji nyota wa vilabu vya AC Milan, Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Robinho, amehukumiwa kufungwa miaka 9 jela na mahakama ya rufaa ya nchini Italia, baada ya kukutwa na kosa la ubakaji wa binti mdogo alilolifanya miaka 7 iliyopoita nchini humo.


Robinho na rafiki yake Ricardo Falco wameripotiwa kumbaka binti huyo raia wa Albania aiishie nchini Italia kwenye kumbi ya starehe wakati binti huyo akiwa anasheherekea mfanano wa siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 23 mwaka 2013.


Wakili wa binti huyo Jaccopo Gnochi amesema '' hukumu hiyo ni mfano kwa wengine juu ya kulinda utu wa mwanake na kuonesha ni jinsi gani mfumo wa sheria unavyofanyakazi''.


Robinho anakumbukwa na wafuatiliaji wengi wa soka ulimwenguni kwa kuwa na uwezo wake mkubwa wa kuuchezea mpira, kuwatoka walinzi kwa chenga kali na kufunga mabao yakuvutia akiwa na vilabu vya AC Milan, Real Madrid, Man city na timu ya taifa ya Brazil miaka ya 2008-13.