Marekani imeiondoa rasmi Sudana katika orodha ya wafadhili waugaidi, kwa mujibu wa ubalozi wake mjini Khartoum.

"Muda wa ilani ya siku 45 iliyowasilishwa kwa bunge la Congress umepita na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametia saini arifa ya kuiondoa Sudan katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi kuanzia leo (Desemba 14), ambayo itachapishwa katika sajili ya serikali," Ubalozi wa Marekani umeandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

Rais wa Marekani Donald Trump mnamo mwezi Oktoba alisema kwamba Sudan itaondolewa katika orodha hiyo baada ya kulipa fidia ya $335m kwa waathiriwa na familia ya shambulio la bomu la al-Qaeda mwaka 1998 dhidi ya ubalozi wa Marekani Afrika.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alijibu kwa kusema fedha hizo zimetumwa.

Sudan iliorodheshwa mwaka1993 wakati kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden alipoishi nchini humo kama mgeni wa serikali. Nchini zingine zilizojumuishwa katika orodha ya kufadhili ugaidi ni Iran, Korea Kaskazini na Syria.