Kwa kawaida ukipewa nafasi ya kutafsiri neno Bongo Fleva na kusema lina maana gani, basi pengine hautacheza mbali sana na maana ile inayofahamika na wadau wengi wa muziki, ya kuwa ni muziki wenye ladha za kutoka hapa kwetu Tanzania.


Kwa @man_water neno hilo halina maana hiyo tena. Akizungumza na kipindi cha Empire cha Efm Radio, producer huyo mkongwe wa muziki hapa nchini, ameeleza namna anavyoitazama maana ya neno hilo 'bongo fleva' na kuwa kwa sasa neno hilo halisimami kujielezea kuwa ni muziki wenye vionjo vya asili ya hapa kwetu, bali limebaki jina tu.


Mtaalam huyo wa kutengeneza midundo, alitoa ushauri pia kwa wasanii na wazalishaji wa muziki kugeukia singeli maana ndio una asili yetu.


“Sasa hivi ni afadhali wasanii na maproducer tuwekeze kwenye singeli na mchiriku kwa maana ukisikiliza ndo utakuta ina ladha ya ngoma za hapa kwetu” amesema @man_water.


Unamtazamo gani juu hili? Tuambie maoni yako