Mwanamke mmoja  mwenye umri wa miaka 29 mkazi wa Uvinza, Kigoma, amekutwa na kuku kwenye kizazi baada ya kufika katika kituo cha afya cha Uvinza, akilalamika kuwa anaumwa tumbo na katika uchunguzi daktari akabaini uwepo wa kifaranga hicho ambacho walifanikiwa kukitoa.

 

Kwa mujibu wa Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Simon Chacha, uchunguzi wa awali, tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina au ukatili kwa maana ya kuku huyo kuingizwa.


“Hakuwa na ujauzito alifika hospitali akadai anaumwa tumbo baada ya uchunguzi madaktari wakaona kifaranga cha Kuku kwenye kizazi na tayari wamekitoa, tukio hilo limefanyika nadhani kwa imani za kishirikina”, amesema Dkt. Simon.


Dkt. Ameongeza kuwa “Nimeagiza afanyiwe upasuaji ili kujihakikishia zaidi nini kimetokea ila kwa kufanyiwa kitendo hicho tayari ameharibiwa kizazi”.Mwanamke asimulia jinsi harusi ilivyompa UKIMWI | East Africa Television