Msanii wa muziki Shilole amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Rommy ambaye aliachana naye miaka 11 iliyopita.

Shilole amedai aliachana na mpenzi wake huyo baada ya kuona hapa pesa na yeye wakati huo alikuwa na majukumu yakulea watoto wake wawili ambao aliwapata katika umri mdogo.

Rommy mwenyewe amethibitisha hilo ikiwa leo Disemba 20, 2020 ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Shilole, ambapo ameeleza kuwa waliwahi kuwa na mahusiano huko nyuma kisha wakaachana.


''Nichukue nafasi hii ya siku yako ya kuzaliwa Shilole kukwambia kua Nakupenda Sana Darling na nashukuru Mungu kwa kutukutanisha tena kwenye maisha yetu ikiwa kila mmoja wetu ameshatimiza malengo yake'', ni sehemu ya ujumbe wa Rommy kwa Shilole.