DAR: Mzazi mwenza wa supastaa wa Bongo Fleva barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Tanasha Donna Oketch, ameonesha waziwazi kuwa, ana kinyongo na ‘mke mwenzake’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

 

Katika mahojiano na chombo kimoja cha habari nchini kwao, Kenya, Tanasha ambaye ni msanii wa muziki wa Kizazi Kipya ndipo alipoonesha hilo mbele ya kamera.

 

Alipoulizwa kuhusu anachompendea mzazi mwenza mwingine wa Diamond au Mondi, mwanamitindo Hamisa Mobeto, Tanasha alijibu kuwa Mobeto anafanya kazi kwa bidii na anajua mno mambo ya fasheni huku akigoma kumzungumzia Zari na kuonesha waziwazi kwamba hapendi kumzungumzia mwanamama huyo, raia wa Uganda.

 

Tanasha anaongeza kuwa, yeye na Mobeto ni wanawake wa shoka kwelikweli kwa hiyo hata wakikutana huwa wanazungumzia zaidi masuala ya kazi na namna ya kuzidi kusapotiana ili kuinuana katika kutoboa kimaisha.

 

Hata hivyo, Tanasha anayedaiwa kuwa mwanamke mzuri zaidi nchini Kenya, alipoulizwa zaidi kwamba kwa nini hapendi kumzungumzia Zari, alikataa katakata kumzungumzia kisha akaekekeza zaidi pongezi kwa Mobeto.

 

Warembo hao wote watatu, Zari, Mobeto na Tanasha kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wamezaa na Mondi na inadaiwa kila mmoja kwa wakati wake alijua angeolewa na jamaa huyo hivyo bado wana hasira na jamaa huyo huku kila mmoja akimuona mwenziye kama adui.

 

Stori: Khadija Bakari