Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma limesema kuwa kuku aliyekutwa kwenye kizazi cha mwanamke mkoani humo, atapelekwa kwenye Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya kuchunguzwa kwani si kawaida kwa binadamu kujifungua kiumbe cha namna ile.

 

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma James Manyama, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, na kusema kuwa tukio la mwanamke huyo kujifungua kuku lilitokea siku ya Desemba 5, 2020, katika kituo cha afya Uvinza.


"Kwa kuwa tukio hili siyo la kawaida kwenye jamii, jeshi la polisi tutachukua kiumbe hicho kwa ajili ya kupeleka Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwani siyo kawaida kwa binadamu kujifungua kuku", amesema Kamanda Manyama.