WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amemvua madaraka Mwenyekiti wa Soko la Madini Chunya na kuwasimamisha kazi watumishi watatu, kufuta leseni za wachimbaji sita wa madini na kuagiza Mawakala wa Wanunuzi wa Dhahabu 13 kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na utoroshaji madini.

 

Maofisa hao ni;

  1. Gabriel Masai
  2. George Wandiba
  3. Edward Gavana.

 

Leseni hizi zinamilikiwa na;

  1. Sabra Habiba
  2. Marofu Said Nasoro
  3. Paul Kheri Nagala
  4. Mashaka Majengo Mwasilini
  5. Yusuf Ferdinand Buyobe
  6. Mabula Mabula.

 

Mhe. Biteko amezifuta leseni hizi kujiusisha na ununuzi wa madini katika masoko yote nchini kuanzia leo Desemba 14, 2020.

 

Aidha, Mhe. Biteko ameagiza kukamatwa kwa mtu anayefamika kwa jina la Frank Mbwilo kwa tuhuma za kununua dhahabu nyumbani kwake kinyume na utaratibu wa uliowekwa wa kununua dhahabu katika masoko ya madini, inadaiwa mbinu hizo ndizo zinatumika kutoroshea madini nje ya nchi.