Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (BAWACHA), wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,CHADEMA, Halima Mdee amesema kuwa uamuzi wakutokuhudhiria  kikao cha kamati kuu ulikuwa ni uamuzi wa busara kutokana na kuwepo kwa mazingira hatarishi.


Akizungumza leo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mdee, amesema kuwa hawakuweza kuhudhuria kikao cha Kamati kuu kutokana na kuwepo na mpango wa kufanyiwa fujo na baadhi ya wanachama huku akisema walimtumia katibu mkuu barua ya kutaka kikao hiko kisogezwe.


“Tuliandika barua ya kutaka kikao hiko kisogezwe tulijibiwa na tulikataliwa na kwa sababau hakukuwa na  mazingira ambayo yalituonyesha zile sababu mbili ambazo tumezitoa zimepatiwa masuluhisho tulidhani kibinadamu ni busara kuto kwenda sio kwamba tulidharau chama wala kikao” amesema Mdee


Aidha kuhusiana na wao kuvuliwa uanachama wao na na nyadhifa zao zote kwenye chama, Mdee amesema kuwa yeye na wenzake wataendelea kuwa wanachama wa chama hicho mpaka rufaa zao zitaposikilizwa.


“Tutabaki Chadema kama wanachama wa hiari, japo tumefukuzwa ila hatutoondoka sisi ni wanachama ving’ang’anizi, hatuondoki Chadema mpaka pale tutakapoenda kusikilizwa rufaa zetu, na tunaamini tutayamaliza na tutaenda kuyajenga ndani kwetu” amesema Mdee.