Muimbaji na mtunzi wa nyimbo hapa nchini, Kassim Mganga ama Gwiji kama anavyojiita kwa sasa, amefanikiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, aitwae Mamu.

Mwimbaji huyo anayesifika kwa tungo za mapenzi, amefunga ndoa hiyo nyumbani kwao Tanga.

Inaelezwa kuwa Mamu na #Kassim ni wapenzi wa siku nyingi hata kabla Kassim hajaanza kung’aa kwenye Bongo fleva.

KassimMganga anaingia kwenye orodha ya mastaa waliofanikiwa kufunga NDOA mwaka 2020, akiwemo mwigizaji Rose Ndauka, msanii Q Chief, Gabo, Esma Platnumz, Asha Boko, Batuli, Haji Manara n.k.