Msanii wa HipHop na Mwanaharakati za kijamii Kala Jeremiah ametoa kali ya mwaka kwa kusema kuna muda hudhani kama yeye sio binaadam wa kawaida kwa sababu ya maono aliyokuwa nayo.


Kala Jeremiah amesema hivyo baada ya kutabiri kuwa wanasiasa wa vyama pinzani hawatarudi wengi Bungeni na kweli imetokea hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.


"Miaka ya nyuma vyama vya upinzani vilikuwa vina nguvu sana kwa sababu ya Agenda Kuu ambazo hata mimi nilikuwa mmoja wanaosapoti ajenda hizo kama Ufisadi na ubadilifu wa mali za Umma ila amekuja Rais ambaye anashughulikia mambo yote hayo"


"Kuna Mheshimiwa mmoja wa upinzani nilikaa naye miezi minne kabla ya Uchaguzi, nikamwambia mna shughuli kubwa sana na wasishangae kama watarudi wachache, mimi nadhani nina maono na sio binadam wa kawaida kuna kipindi nahisi nilikufaga sehemu huko kwenye karne ya 15" ameongeza 


Aidha msanii huyo amesema kama Mungu atamuweka hai mwaka 2025 atatia nia ya kugombea Ubunge maana amepata msukumo mkubwa kutoka kwa watu ambao wanataka afanye hivyo.