MASKINI! Mkali wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ameweka wazi kuwa kutokana na umri alionao wa miaka 38, ameshakata tamaa ya kuzaa mtoto mwingine tena hivyo atabaki na mwanaye Paula tu.


Kajala aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, kipindi cha nyuma alikuwa akisaka mtoto mno, lakini ilishindikana hivyo umri unasogea na pia mtoto wake ameshakua ni msichana mkubwa hivyo inabidi aangalie maisha mengine na siyo kuzaa tena.


“Nilitamani sana kupata hata watoto wawili, lakini ilishindikana kwa wakati, hivyo nimeona bora sasa kuangalia kitu kingine mbele maana nimekata tamaa kabisa ya kuongeza mtoto mwingine, ninajikita kwenye kumuwezeshe Paula asonge mbele kielimu,” alisema Kajala kwa masikitiko.