IMEFAHAMIKA kuwa, upo uwezekano mkubwa wa mastaa wanne kuondoka na wengine kutoongeza mikataba ya kuendelea kuichezea Simba pindi usajili wa dirisha dogo msimu huu utakapofi ka, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck akitajwa ndiyo sababu.Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu na kufungwa Januari 15, mwakani ambapo timu za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi Daraja la Pili na Ligi Kuu ya Wanawake zitafanya usajili wa kuboresha vikosi vyo.

 

Simba imepanga kukiboresha kikosi chake katika dirisha dogo kwa kusajili mshambuliaji mmoja wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kufunga na beki, huku ikiwa tayari imemsajili kiungo mkabaji kutoka Uganda, Taddeo Lwanga aliyepewa mkataba wa miaka miwili.



Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere

ndiye mchezaji wa kwanza aliyeomba kutoongozewa mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo akidaiwa kutokuwa na maelewano mazuri na Sven.

 

Mtoa taarifa huyo aliwataja wachezaji wengine ni Miraji Athumani ‘Sheva’, Charles Ilanfya na Gadiel Michael baada ya wote hao kukosa nafasi ya kucheza.Aliongeza kuwa, Sheva nafasi yake imekuwa ndogo ya kucheza tangu alipopata majeraha msimu uliopita pamoja ushindani aliokutana nao kutoka kwa Luis Miquissone, Clatous Chama, Bernard Morrison, Larry Bwalya na Francis Kahata.

 

“Wachezaji wenyewe wameomba kuondoka Simba baada ya kocha Sven kuonekana kutowahitaji katika timu yake.“Kati ya hao ni Kagere, kama unakumbuka vizuri tangu mwanzoni mwa msimu huu kocha ameonekana kumuweka benchi huku akimpa nafasi ya kucheza Bocco (John) ambaye kwake ni chaguo la kwanza na hivi karibuni alitamka hivyo.“Lakini pia yupo Ilanfya aliyejiunga na Simba msimu huu ambaye tangu amefi ka ameoneakana kutompa nafasi ya kucheza, huyu alishaomba kurejeshwa KMC kwa mkopo.

 

“Sheva naye ni kati hya wachezaji watakaoondoka, ingawa bado taarifa yake rasmi haijakwenda kwa uongozi. Na yeye shida ni hiyohiyo hapati nafasi, anataka kwenda kulinda kipaji chake baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha aliyoyapata katikati ya msimu uliopita,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Simba, Anorld Kashembe kuzungumzia hilo, alisema: “Jukumu la usajili lipo kwa kocha kwani yeye ndiye anayependekeza usajili wa wachezaji wapya na wale wa kuachwa. Tusubiri muda ufi ke kila kitu kitawekwa wazi.