Jumba kubwa la kifahari la Neverland alilokuwa akiishi Mfalme wa Pop marehemu Michael Jackson huko Los Olivos, California limeuzwa kwa bilionea Ron Burkle ambaye ni rafiki wa zamani wa Michael Jackson kwa $22M (sawa na bilioni 51 za Kitanzania) ambayo ni robo ya thamani kwani kwa mara ya kwanza lilinadiwa kwa $100M mwaka 2015.


Michael Jackson alilinunua jumba hilo mwaka 1987 kwa $19M na kulifanya kuwa nyumbani kwake wakati wa umaarufu wake na alibadilisha jumba hilo na kuwa eneo la burudani, akijenga eneo la kufuga wanyama mbali, ukumbi wa chini ya ardhi na maeneo ya kuchezea watoto na familia zao


Jumba hilo lililonunuliwa na bwana Ron Burkle limejengwa katika shamba la ekari 2700 na tayari limebadilishwa jina na kuitwa Sycamore Valley Ranch. Jumba hilo limefanyiwa ukarabati mkubwa tangu kufariki kwa Michael Jackson Mwezi June 2009.