Jay-Z amezidi kukolezwa na muziki wa Burna Boy toka nchini Nigeria, ameitaja ngoma yake kwa mara nyingine tena kwenye orodha ya mikwaju mikali iliyofanya vizuri kwenye masikio yake kwa mwaka 2020.


Orodha hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wake wa TIDAL, Jay-Z ameitaja ngoma ya Burna Boy "Onyeka (Baby)" toka kwenye album ya #TwiceAsTall ya mwaka huu.


Kuonesha kwamba anauzimia sana muziki wa Afrika, Jigga ameitaja pia ngoma ya Master KG "Jerusalema" Remix ambayo pia Burna Boy ameshirikishwa. Hizi ndio ngoma mbili pekee kwenye list ya mikwaju heavy na pendwa kwa Jay-Z mwaka huu.


Mwaka jana kwenye Playlist yake, Jay-Z aliitaja ngoma ya Burna Boy "Collateral Demage" toka kwenye album ya African Giant.