MMOJA wa mastaa wakali wa filamu Bongo, Irene Uwoya amesema kuwa hakuna kitu ambacho hajakifurahi kwenye moyo wake kama mdogo wake,kuwa kwenye uhusiano na rafiki yake pia msanii mwenzie Mariam Ismail ‘ Mama kubwa’ na hata anapowaona uwa anakereka sana.

 

Akizungumza na Ijumaa, baada ya kuonekana kwenye kipindi chake Cha ‘Im very Woman, akilalamika,Uwoya aliliambia gazeti hili kuws hakuna kitu anachotamani kukivunja kama uhusiano huo ambao umeshafika mbali sana na Sasa hivi wanataka kuoana.“

Niwe tu mkweli hakuna mahusiano ambayo sipendi kama ya mdogo wangu na Mariam, yaani sina furaha nayo na siyapendi kabisa na uzuri wanalijua hilo wote wawili, na pia uhusiano huo umefanya sasa nisiwe karibu kabisa na Mariam, Kama ilivyokuwa huko nyuma’ alisema Uwoya.


 

Gazeti hili lilipomtafuta Mariam, kwa upande wake alisema kuwa siku zote hakuna mtu anayewazuia watu wawili wanaopenda hata siku moja.“

 

Unajua ni ngumu sana watu wanaopenda kuwazuia kwa chochote kwasababu moyo ukishapenda ni ngumu kuupangia kupenda mwingine” alisema Mariam.

 

Mariam na Uwoya,ni marafiki wa muda mrefu sana,lakini sasa hivi ni wifi yake kwa mdogo wake wa pekee anayeitwa babuu.