Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaonya baadhi ya wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na hasa kwa kufunga barabara kwa kuweka mawe na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

IGP Sirro amesema hayo jana akielekea mkoani Arusha na kulazimika kusimama katika kijiji cha Kelema wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kutokana na kitendo cha wananchi kufunga barabara kuu ya Dodoma, Babati kufuatia kuchoshwa na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika eneo hilo na kusababisha vifo na majeruhi.

Akizungumza kwa niaba ya wanakijiji hao BiKulusumu maarufu mama Kibibi amemuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Sirro kuwawekea askari wa kutosha wa usalama barabarani pamoja na kuweka matuta na beria itakayosaidia kupunguza ajali.