Mchekeshaji @idrissultan ambaye pia ni mfanyabiashara hapa Bongo amedai kuwa amefanikiwa kizirejesha Dola Laki 3 (zaidi ya Milioni 500) alizoshinda Big Brother Africa mwaka 2014 nchini Afrika Kusini.


Inaelezwa fedha hizo zilipotea baada ya kuwekeza kwenye miradi ambayo haikuweza kuzaa matunda kutokana na kukosa uangalizi mzuri, huku mwenyewe akidai watu wake wa karibu ndio waliomwangusha.


Akizungumza na kipindi cha Empire cha E FM Redio, #Idris amesema fedha hizo alifanikiwa kuzirejesha rasmi mwaka 2018 baada ya kufanya kazi kwa bidii na kuanzisha miradi mbalimbali.


“Ile dola laki tatu, nimekuja kuipata tena 2018, hiyo ni miaka minne baadaye, siku hiyo naenda Benki wananiambia umetimiza dola laki tatu yako, wakaanza kunipigia makofi, ndio maisha,” amesema @idrissultan


Ameongeza kuwa alipoenda Big Brother hakuwa ni mpango kupata fedha, bali kupata platform, halafu aitumie kufanya vitu vyake vikubwa sana na ndio kitu nafanya hadi sasa.