Mchambuzi wa soka nchini, Abbas Pira amezungumzia uzito wa mchezo wa wawakilishi wa nchi katika Klabu bingwa Barani Afrika Simba dhidi ya FC PLatnum na kudai kuwa kwa mtazamo wake Mnyama Simba watapata matokeo mazuri ya magoli matatu (3) kutokana na wapinzani wao kutokuwa na kikosi cha kutisha.

”Simba watapata matokeo jijini Dar Es Salaam, hawa jamaa FC Platnum ni wakawaida sana. Kwangu mimi Simba atashinda magoli 3 Dar Es Salaam.”