Rais wa Marekani Donald Trump hatimaye ameusaini muswada wa sheria wa dola bilioni 900, unaokusudia kutoa misaada kwa watu walioathiriwa na janga la virusi vya corona, pamoja na bajeti ya serikali ya shirikisho ya dola trilioni 1.4. 

Awali, Rais Trump alikataa kutia saini muswada huo tangu ulipopitishwa na bunge wiki iliyopita. 

Kulikuwa na wasiwasi kuwa kuchelewa kufanya hivyo, baadhi ya faida za ukosefu wa ajira zingepotea, na kwamba mamilioni ya watu wanaweza kupoteza pesa katikati mwa ugumu wa kiuchumi uliochangiwa na janga la virusi vya corona.

 Trump alitaka baadhi ya vipengele vya matumizi, ikiwemo misaada ya kigeni kuondolewa katika bajeti. 

Rais huyo hakusema kwanini ameamua kutia saini sheria hiyo lakini saa chache kabla ya kuusaini aliandika katika Twitter kwamba watu watarajie habari njema. 

 

-DW