Msanii Bright Music amesema wasanii wazingatie zaidi kwenye suala la kazi isiwe kwenye mambo ya kiki au 'trending' kwa sababu utandawazi umeleta vitu vingi ikiwemo kurahisha na kuwaharibia.

Bright Music amezungumza hayo kufuatia 'show biz' wanazofanya wasanii wa BongoFleva ikiwemo suala la  Marioo kusema ameweka meno ya dhahabu nchini Afrika Kusini ambayo yana thamani milioni 7.

"Tu-focus zaidi kwenye kazi mambo ya kiki na ku-trend sio vitu vibaya kwa mtu ambaye anatumia na vinampa faida, Marioo kapata pesa acha afanye anachojisikia maana ukiwa na pesa unaweza ukaamka ukatembea na boxer halafu unaweza ukasema umeinunua bilioni 7, mtu akiwa na pesa jeuri yake inaongea" ameeleza Bright