Msanii H Baba amesema amepata baraka zote kutoka kwa mama yake baada ya kuweza kumjengea mzazi wake huyo nyumba ya tatu iliyopo Nyasaka Jijini Mwanza, ambapo mjengo huo una thamani ya shilingi milioni 200.

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, H Baba amesema anatokea kwenye familia ya kimaskini kwa hiyo mama yake hakuwa na furaha pia hajawahi kumfanyia kitu au jambo kubwa ndiyo maana amem-surprise kwa mjengo huo.


"Mimi natokea kwenye familia ya kimaskini mama hakuwa na ile hali ya furaha kwa sababu nilikuwa sijawahi kumfanyia kitu kikubwa, nilichofanya ni kumjengea nyumba ya kwanza akapangisha ya pili akasema ipo mbali na Jiji hivyo hawezi kuishi peke yake ndiyo maana nikamjengea hii ya tatu" amesema H Baba 


H Baba ameongeza kusema mjengo huo umechukua muda wa miezi mitano hadi kukamilika kwake na ina thamani ya milioni 200.