MWANAMAMA anayefanya vizuri kwenye Bongo Fleva, asiyeishiwa makeke, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ameshangaa mno kusikia eti kinara wa muziki huo barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo singo!

 

Kwa mujibu wa Gigy, haamini hata tone kama Diamond au Mondi hana mpenzi hivyo kuwataka wanaoamini hivyo waache hizo.

Gigy anasema kuwa, mtu kama yeye au Mondi siyo watu wa kuweza kuwa singo, lakini kinachotokea ni kwamba hawajapenda tu kuweka mambo yao wazi.

“Mimi nipo singo? Diamond yupo singo? Acheni hizo bwana, labda kama tu hajaamua kuweka in public (hadharani).

“Yaani Diamond kabisa akae miezi bila ku…(mguno na kicheko cha kejeli.

 

“Mimi nikae singo kwani hicho…(neno lisiloandikika gazetini) ninacho cha nini?” Anahoji Gigy mara baada ya kusambaa kwa picha zake na Mondi zikiwaonesha kama mtu na mtuwe, walipokuwa jijini Arusha.

Gigy na Mondi wanatajwa kuwa ni marafiki wakubwa ndiyo maana katika moja ya nyimbo zake maarufu, Mondi anasikika akisema; “Mwanangu Gigy sikuoni!”

 

Katika shoo na matukio mbalimbali ya Wasafi, Gigy amekuwa hakauki.

Inaelezwa kwamba, Mondi huwa anapenda ‘haso’ za Gigy za kutoboa kimuziki tangu kitambo hicho hivyo ukaribu wao ni aina fulani ya kuoneshana sapoti kati yao na wala hakuna suala la mapenzi kama baadhi ya mitandao inavyovumisha.

 

Hata hivyo, kauli ya Gigy inaonesha kuwa, kuna kitu anakijua juu ya maisha ya kimapenzi ya Mondi. Huwenda anajua Mondi ana mpenzi hivyo kuwashangaa wanaoamini kwamba yupo singo.

 

Miezi kadhaa iliyopita, Gigy aliposti picha akiwa na Mondi kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo alieleza dhahiri kuwa, anamzimikia mno jamaa huyo ambaye ni baba wa watoto wanne.

 

Katika moja ya intavyu nyakati hizo, Gigy aliliambia Gazeti la IJUMAA kwamba, ni kweli anatamani kutoka kimapenzi na Mondi na wala hajali kama yeye ana familia.

 

Katika mahojiano hayo, alisema Mondi alikwishaonesha utayari wa kutoka naye kimapenzi ila mambo mengine yanatakiwa kubaki kuwa siri yao.

Stori: Imelda Mtema