GARI la mwanamuziki maarufu nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘DiamondPlatnumz’, limemzulia jambo zito na kumuweka katika ‘vita ya maneno’ Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi. vita hiyo imekuja kufuatia Rais Tshisekedi kuonekana na gari la aina ambayo linamilikiwa na Diamond au Mondi.

LINA THAMANI YA MIL. 200

Gari hilo aina ya Toyota Landcruiser VX57, linakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni 200 za Kitanzania na linatumiwa pia na Rais huyo wa Kongo katika misafara yake.

Novemba 20, mwaka huu, Diamond au Mondi aliibua mjadala nchini Kongo kuhusu gari hilo, baada ya kutupia picha kwenye ukurasa wake wa Mtandeao wa Instagram akiwa amesimama mbele ya gari hilo.

Licha ya Mondi kutozungumza lolote kuhusu mjadala huo unaoendelea huko nchini Kongo, baadhi ya raia wa Kongo walianza kumlinganisha Mondi na Rais Tshisekedi ambaye mara kwa mara alionekana na gari hilo kwenye baadhi ya misafara yake

WANAOMILIKI GARI HILO NI HAWA

Kwa mujibu wa Mtandao wa Internationalnewsblog, Rais Tshisekedi anakuwa mtu wa tatu kumiliki gari la thamani hiyo nchini humo.

Mbali na Rais Tshisekedi, mwingine anayedaiwa kuwa na gari la aina hiyo huko Kongo ni Mchungaji Joel Francis Tatu

ambaye Oktoba, mwaka huu alidai kuwa alipewa gari hilo kama zawadi kutoka kwa mfadhili mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake wa tatu anayetajwa kuwa na la gari aina hiyo nchini humo ni mwimbaji maarufu wa muziki wa Lingala, Herve Ngola Bataringealmaarufu Ferre Gola ambaye anaungana na Mondi pamoja na tajiri namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kumiliki gari la aina hiyo.