Usiku wa kuamkia leo Jumatatu 21-12-2020 lilifanyika tukio kubwa la utoaji tuzo nchini Marekani, ambapo Kumetolewa tuzo za #aeausa2020 ambapo katika tuzo hizo Wasanii watatu wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Tanzania yaani Diamond Platnumz, Rayvanny na Nandy wamefanikiwa kushinda tuzo hizo kwenye vipengele tofauti tofauti.
Mbali na Diamond Rayvanny na Nandy kushinda tuzo pia DJ Sinyorita kutoka Clouds Fm amefanikiwa kushinda tuzo ya DJ bora.
Diamond ametangazwa mshindi tuzo za @aeausa 2020 katika kipengele cha “Best Male Artist” (Msanii Bora wa Kiume) akiwashinda Eddy Kenzo, Wiz Kid , Shatta Wale, Stonebwoy, Davido, Burna Boy, Mohamed Abbas, Fally Ipupa na Jahllano ambao alikuwa akichuana nao kwenye Kipengele hicho.
Huku Rayvanny akitangazwa mshindi tuzo za @aeausa 2020 katika kipengele cha Best Male Artist – East/South and North Africa akiwashinda Elgrande toto, The Ben, Diamond Platnumz, Alikiba
Eddy Kenzo, Harmonize, Tewodros kassahun AKA Teddy Afro, Jah Prayzah na Bruce Melodie.
Kwa upande wa Nandy ametangazwa mshindi tuzo za @aeausa 2020 katika kipengele cha “Best Female Artist” akiwashinda Zahara, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sho Madjozi
,Sha Sha, Sheebah Karungi, Rema Namakula, Aya Nakamura na Kenza Morsli .
DJ pekee kutoka Tanzania DJ Sinyorita ameshinda kipengelea cha DJ bora akiwashinda DJ Moh
2. DJ Cuppy
3. DJ Slick Stuart & DJ Roja
4. DJ Shimza
5. DJ Nelasta
6. DJ Tunez
7. DJ Xclusive
8. DJ K Meta
9. DJ Roma
Hii hapa chini ni orodha ya washindi wote wa tuzo hizo.
1. Best Male Artist: Diamond platinumz
2. Best Female Artist: Nandy
3. Best Hip Hop/Rap Artist: Elgrande Toto
4. Hottest Group: Sauti Sol
5. Best Collaboration: Beyonce ft Shatta Wale – King Already
6. Best Music Video: Burnaboy – Anybody
7. Entertainer of the Year: Eddy Kenzo
8. Best Dancer/Group: Fire K Stars
9. Best DJ: DJ Sinyorita
10. Best Francophone Artist: Soul Bangs
11. Best Palop Male Artist: Mr Bow
12. Best Palop Female Artist: Yasmine
13. Best New Artist: Laycon
14. Song of the Year: Master KG – Jerusalema
15. Best Upcoming/Local Artist: KG
16. Best Male Artist – Central/ West Africa: Stonebwoy
17. Best Male Artist – East/South/North Africa: Rayvanny
18. Best Female Artist- Central/ West Africa: Yemi Alade
19. Best Female Artist – East/South/North Africa: Zahara
20. Best African Comedian: Eric Omondi
21. Best Gospel Artist: Sinach
22. Best Blogger/ Influencer: The Hot Jem
23. Best Dance Hall Artist: Winky D
24. Best Host TV/ Radio: Douglas Lwanga