Nyota wa muziki wa Bongo Fleva Elias Barnaba, maarufu Barnaba ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki, hatimae leo ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Katika kuelekea kuumaliza mwaka 2020, Barnaba awabariki mashabiki zake na "Refresh Mind" yenye jumla ya ngoma 14, ikiwa na kolabo 6 pekee. Ameshirikiana na wasanii mbalimbali wa ndani ya nchi akiwemo Mimi Mars, Dogo Janja, G Nako, Country Wizzy, Nikki wa Pili, Malkia Karen, Linah na Christian Bella.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Barnaba amemshukuru Mungu kwa kuweza kuikamilisha Album hiyo na hatimae kuitoa, "Asante mwenyezi MUNGU - haikua rahisi Lakini kwasababu ya Neema zako Tu Final my 𝐀𝐋𝐁𝐔𝐌- 𝐈𝐒 -𝐎𝐔𝐓 Now 💽 #𝐑𝐄𝐅𝐑𝐄𝐒𝐇𝐌𝐈𝐍𝐃𝐀𝐋𝐁𝐔𝐌💽🕊"

                                            DONWNLOAD HERE